Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maandalizi na uratibu wa mapema ni muhimu kwa ugawaji misaada:Holmes

Maandalizi na uratibu wa mapema ni muhimu kwa ugawaji misaada:Holmes

Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa kuratibu masuala ya misaada ya kibinadamu John Holmes ameliambia baraza la uchumi na jamii linalokutana mjini New York kuwa tunahitaji kutambua wapi ambako misaada ya kibinadamu ni lazima ipelekwe.

Ameongeza kuwa ni muhimu kujua jinsi gani ya kukabiliana na matatizo, kuliko kujikita katika matatizo ya kushtukiza ndio hatua zichukuliwe. Amesema ongezeko la athari za mabadiliko ya hali ya hewa, majanga ya asili, msukosuko wa kiuchumi na vita vimeongeza mara dufu mahitaji ya misaada ya kibinadamu.

Holmes amesema kutoka na ripoti ya katikati ya mwaka huu 2010 maombi ya msaada yameongezeka na kufikia thamani ya dola bilioni 8.5 kuwasaidia watu milioni 53, ikilinganishwa na mwaka 2009 ambapo waliotaka kusaidiwa ni watu milioni 43. Hata hivyo amesema anafuraha kwamba juhudi zao zinaendelea.

(SAUTI YA  HOLMES ECOSOC)