Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Global Fund na watengeneza dawa za malaria waafikiana kupunguza bei kwa asilimia 80

Global Fund na watengeneza dawa za malaria waafikiana kupunguza bei kwa asilimia 80

Mfuko wa kimataifa yaani Global Fund na makampuni yanayotengeneza dawa za malaria zenye ubora wamekamilisha makubaliano ya kupunguza bei ya dawa za malaria ili mamilioni wanaozihitaji waweze kumudu hususani watoto.

Mpango huu wa ushirikiano wa umma na makampuni binafsi ni sehemu ya mpango wa uwezeshaji wa upatikanaji wa dawa za malaria AMFM duru ya kwanza na utaokoa maisha ya watu na kuzinufaisha nchi nane za Afrika zilizo kusini mwa jangwa la Sahara na Asia. Chini ya makubaliano hayo waingizaji binafsi wa dawa sasa watalipa katika bei ya punguzo hadi la asilimia 80 ikilinganishwa na mwaka 200 hadi 2009 kwa dawa zilizobora zaidi za kutibu malaria kama artemisinin na hivyo kupunguza pia bei ya viwandani na kwa wanunuzi wa sekta za umma.

Mkurugenzi mtendaji wa Global Fund Michel amesema makubliano haya yanasogeza karibu ndoto za siku ambapo kila mtu anayetaka dawa ya malaria aweze kumudu kuinunua. Amewashukuru wahusika wote kwa ushirikiano, wadau, makampuni ya kutengeneza dawa, na uongozi bora wa nchi mbalimbali, na kusema sasa watavifanya vifo vya malaria kuwa historia.