Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na chuo kikuu cha oxford wametoa vielelezo vipya vya kupima umasikini

UM na chuo kikuu cha oxford wametoa vielelezo vipya vya kupima umasikini

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo UNDP na chuo kikuu cha Oxford leo wamezindua vielelezo vipya vya kupinma kiwango cha umasikini.

Wanasema vielelezo hivyo vinatoa taswira ya Nyanja mbalimbali kwa watu wanaoishi katika mazingira magumu na vinaweza kusaidia kulenga rasilimali za maendeleo kwa urahisi zaidi. Vielelezo hivyo vipya MPI vimeandaliwa na kujaribiwa na chuo kikuu cha Oxford na mpango wa maendelep OPHI kwa msaada wa wa UNDP.

Zikizungumza na waandishi wa habari taasisi hizo mbili zimesema vielelezo hivyo jumuishwa katika toleo la 20 la ripoti ya UNDP ya maendeleo ya binadamu na vitachukua nafasi ya ripoti ya umasikini ambayo imekuwa ikijumuishwa katika ripoti hizo tangu mwaka 1997. Kipimo kinaonyesha aina na kiwango cha umasikini katika ngazi mbalimbali, kuanzia nyumbani, kimkoa, kitaifa na kimataifa.