Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Homa ya kidingapopo imesambaa Kusini mwa Yemen na kuathiri watu wengi

Homa ya kidingapopo imesambaa Kusini mwa Yemen na kuathiri watu wengi

Homa ya vipindi au kidingapopo inayosambazwa na mbu imeyakumba maeneo ya kusini na mashariki mwa Yemen.

Kwa mujibu wa serikali maeneo yaliyoathirika zaidi na homa hiyo ni Hadhranaut, Taiz, Aden na Abyan ambako watu wengi wamekufa na idadi inaongezeka. Taarifa za wizara ya afya ya nchi hiyo zinasema homa hiyo inasambaa haraka katika mji wa Mukalla ambako watu 12 wamekufa na wengine 1442 wameathirika na homa hiyo tangu Aprili.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO homa ya kidingapopo kwa mara ya kwanza ilibainika Yemen miaka ya 1990 na imekuwa ikizuka mara kwa mara kuanzia hapo. Dalili za homa hiyo ni pamoja na homa kali, kutapika, kuumwa kichwa, ochovu na kuvuja damu.