Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada zaidi na wa haraka unahitajika eneo la kaskazini mwa Mali

Msaada zaidi na wa haraka unahitajika eneo la kaskazini mwa Mali

Mkuu wa shirika la lisilo la kiserikali la misaada Oxfam nchini Mali Gilles Marion amesema mashirika ya misaada yanashindwa kufikia mahitaji ya maji na chakula kwa watu na mifugo walioathirika na ukame nchini humo.

Kwa mujibu wa kitengo cha tahadhari cha serikali , watu 258,000 wanahitaji msaada wa haraka, na wengine 371 wako katika hatari kufuatia mvua hafifu za masika kwenye eneo hilo la Sahel. Kuna utapia mlo uliokithiri wa asilimia 19, asilimi 40 ya mifugo katika eneo la kaskazini inaumwa au imekufa na mingine asilimia 30 iko katika hatari ya magonjwa au kufa kutokana na ukosefu wa chakula.

Shirika la mpango wa chakula WFP, shirika la chakula na kilimo FAO, kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC na Oxfam ni miongoni mwa mashirika yanayotoa msaada wa dharura miji ya Gao na Kidal.

Oxfam inasema endapo hatua za haraka na misaada haitopelekwa hivi karibuni basi hali itakuwa mbaya zaidi na maisha ya watu kupotea.