Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kutoweka kwa mikoko kunaathiri uchumi wa dunia na maisha:UNEP

Kutoweka kwa mikoko kunaathiri uchumi wa dunia na maisha:UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP limesema tathimini ya kwanza ya kimataifa kwa zaidi ya muongo mmoja kuhusu mikoko inaonyesha kwamba mikoko inaendelea kutoweka.

Kwa mujibu wa kitabu cha ramani cha dunia licha ya juhudi za kuboresha mikoko katika baadhi ya nchi bado mimea hiyo adimu inapotea.Tathimini ya kiuchumi inatoa hoja muhimu ya kuunga mkono kuitunza, kuilinda na kuikarabati mikoko, kwani utafiti umebaini kuwa mikoko inaingiza kati ya dola 2000 hadi 9000 kwa ekari moja kwa mwaka, ikiwa ni kiwango kikubwa kuliko faida ya kilimo au utalii.

Takribani moja ya tano ya mikoko yote imearifiwa kutoweka tangu mwaka 1980. Ingawa kiwango cha kutoweka ni kidogo lakini wataalamu wameonya kwamba ongezeko lolote la kutoweka kwa mikoko hiyo litakuwa na athari kubwa kwenye uchumi.