Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baada ya mashindano ya kombe la dunia Afrika ndio washindi hasa:UM

Baada ya mashindano ya kombe la dunia Afrika ndio washindi hasa:UM

Umoja wa Mataifa umepongeza michuano ya kombe la dunia mwaka huu wa 2010 na kusema imekuwa mafanikio makubwa kwa pande zote husika.

Umoja wa Mataifa umesema pamoja na kuheshimu matokeo ya fainali, lakini lakini washidi hasa wa kombe hilo ni Afrika na watu wa Afrika. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye alihudhuria ufunguzi wa mashindano ya kombe la dunia amesema hakuna shaka kwamba mashindano ya kombe la dunia yamekuwa ni mafanikio makubwa kwa Afrika ya Kusini na bara zaima la Afrika.

Naipongeza serikali na watu wa Afrika Kusini. Ni matumaini yangu kwamba mtazamo huu kwa Afrika utaleta matumaini na mabadiliko katika bara hilo.