Skip to main content

Katika msaada wote ulioahidiwa Haiti ni asimilia mbili tuu iliyopatikana

Katika msaada wote ulioahidiwa Haiti ni asimilia mbili tuu iliyopatikana

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti amesema kati ya dola bilioni 10 za msaada wa ujenzi mpya zilizoahidiwa ni asilimia mbili tuu iliyopatikana.

Mwakilishi huyo Leslie Voltaire ameyasema hayo kwenye kikao maalumu cha baraza la jamii na uchumi kilichokuwa kikijadili juhudi za kuitoa Haiti katika msaada wa dharura kwenda katika ngazi ya maendeleo na ujenzi mpya. Amesema bado Haiti haijaingia kwenye hatua ya ujenzi mpya, hakuna tofauti kati ya waathirika wa tetemeko na wale wanaokabiliwa na umasikini uliokithiri.

(SAUTI YA LESLIE HAITI)

Serikali iliweka mipango maalumu ya kuratibu misaada lakini juhudi za kubadilishana taarifa imekuwa tatizo kubwa.