Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajira kwa vijana ni mgogoro mkubwa lasema shirika la kazi duniani ILO

Ajira kwa vijana ni mgogoro mkubwa lasema shirika la kazi duniani ILO

Ripoti ya shirika la kazi duniani ILO inasema vijana wameathirika vibaya na matatizo ya uchumi yaliyoikumba dunia kuanzia mwaka 2008.

Ripoti hiyo iitwayo ajira ya vijana katika matatizo, inasema hali hii imeongeza changamoto zilizokuwepo awali na kuna hofu kwamba kama hatua hazitochukuliwa basi hali ya vijana itakuwa mbaya zaidi na kuweka mfumo mzima wa jamii katika tisho kubwa.

Tangu kuanza kwa mgogoro wa kiuchumi kiwango cha ukosefu wa ajira kwa vijana kimepanda zaidi ya asilimia saba, ambacho ni kikumbwa sana katika muda wa miaka miwili ukiangalia historia. Na sasa kimezidi asilimia 21 kwa wastani wa nchi ambazo takwimu zake zimepatikana.