Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afrika Magharibi bado iko njia panda licha ya hatua zilizopigwa:UM

Afrika Magharibi bado iko njia panda licha ya hatua zilizopigwa:UM

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa Afrika ya Magharibi amesema chanzo cha migogoro ya eneo hilo ikiwa ni pamoja na mivutano ya kikabila na changamoto za kiutawala vinaweza kubadili hatua zilizopigwa kuleta amani eneo hilo na kuuacha ukanda mzima njia panda.

Mwakilishi huyo Said Djinnit ameyasema hay oleo mbele ya baraza la usalama na kusema msaala wa jumuiya ya kimataifa lazima uendelee kutolewa ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa kuendelea kuchagiza juhudi za amani na utulivu.

Miezi sita baada ya taarifa ya mwisho ya bwana Djinit kwenye baraza la usalama amesema hali imeanza kuimarika lakini mapema mwaka huu mvutano wa katiba ulikuwa unatokota Niger, huku maisha ya maelfu ya watu yakiathirika na upungufu wa chakula , usafirishaji haranmu wa mihadarati na vikwazo vingine nchini Guinea.

Anasema hata hivyo kufanyika kwa uchaguzi wa amani Togo ,kuundwa kwa serikali na kushiriki kwa upinzani pamoja na serikali ya mpito Niger kunatia matumaini. Ameongeza kuwa hatua zitakazopigwa Guinea zitasaidia kutatua migogoro ya nchi jirani ya Guinea-Bissau ambayo inaghubikwa na mivutano ya kisiasa hivi sasa.