Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna hatua katika utekelezaji wa azimio kwa Israel na Lebanon:UM

Hakuna hatua katika utekelezaji wa azimio kwa Israel na Lebanon:UM

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo inasema ingawa Israel na Lebanon wamekuwa na utulivu wa muda mrefu katika historia ya karibuni ,hakuna hatua kubwa waliyopiga katika majukumu muhimu ya azimio la baraza la usalama lililomaliza machafuko mwaka 2006.

Ili kumaliza vita vilivyozuka baina ya Israel na kundi la Hizbollah la Lebanon miaka mine iliyopita, azimio namba 1701 la baraza la usalama limetoa wito wa kuheshimu linachokiita mstitari wa bluu unaotenganisha Israel na Lebanon, kuyapokonya silaha makundi yote ya wanamgambo ya Lebanon na kukomesha uingizaji haramu wa silaha katika eneo hilo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ripoti yake anasema ingawa pande zote mbili zimejidhatiti kutekeleza azimio 1701 kumekuwa na ukiukwaji kadhaa na hakuna hatua iliyoarifiwa ya utekelezaji wa majukumu muhimu kwa kuzingatia azimio hilo.