Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano mapya Kivu Kaskazini DR Congo yawafungisha virago maelfu

Mapigano mapya Kivu Kaskazini DR Congo yawafungisha virago maelfu

Mapigano mapya baina ya vikosi vya serikali ya Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo na kundi la waasi wa Uganda yamewafanya watu takribani 20,000 kukimbia vijiji vyao kwenye jimbo la Kivu ya Kaskazini.

Habari hizi ni kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo inasema idadi ya walioachwa bila makazi na mapigano baina ya serikali na kundi la Allied Democratic Forces ADF ni ndogo, ikilinganishwa na watu milioni 1.8 ambao ni wakimbizi wa ndani. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA watu kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine sio jambo la busara kwa sababu hadi sasa mji wa Beni Kivu Kaskazini umeweza kuhifadhi wakimbizi wa ndani 10,000 pepkee.

OCHA inasema watu waliosambaratishwa na machafuko wiki jana baina ya vikosi vya serikali na ADF ni wa kwanza tangu mwaka 2006, na inahofia athari za mapigano hayo kwa raia. Mashirika ya misaada ya kibinadamu yanakisia kwamba watu wapatao 14,000 wanahitaji msaada wa dharura ikiwa ni pamoja na chakula, malazi, maji, na madawa.