Marekani kufikiria udhibiti wa silaha za angani kwa ajili ya usalama
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Marekani Frank Rose akizungumza kwenye mkutano wa upokonyaji silaha leo mjini Geneva amesema Marekani itafikiria kuhusu udhibiti wa silaha za angani.
Rose amesema nchi yake mbali ya masuala yanayohusiana na udhibiti wa silaha za angani, pia itafikiria mapendekezo ya kufikia vigezo vya usawa na udhibiti, ambavyo vitasaidia usalama wa taifa wa Marekani na washirika wake.
Pia amesema Marekani inazitaka nchi zote kutambua kwamba wote wana haki ya kutumia anga kwa amani kwa faida ya wote.
(SAUTI FRANK ROSE)