Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama la UM limelaani mashambulizi ya mabomu Uganda

Baraza la usalama la UM limelaani mashambulizi ya mabomu Uganda

Baada ya kufanyika shambulio la mabomu mjini Kampala Uganda siku ya Jumapili polisi wamekamata ukanda unaovaliwa na mlipuaji wa kujitoa muhanga kwenye klabu ya usiku Jumatatu mchana.

Watu zaidi ya 70 waliuawa kwenye shambulio la Jumapili wakati wakiangalia fainali za kombe la dunia, wengine wengi kujeruhiwa na sasa watu kadhaa wanashikiliwa na polisi. Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupitia Rais wake wa mwezi huu balozi wa Nigeria U. Joy Ogwu limelaani vikali na kusisitiza haja ya kuwafikisha wahusika kwenye vyombo vya sheria.

(SAUTI YA JOY OGWU)

Baraza hilo limewataka wajumbe wote 15 kushirikiana na serikali ya Uganda katika kukabiliana na tatizo hilo. Kundi la wanamgambo wa Kiislamu kutoka Somalia Al-Shabab limdai kuhusika na mashambulio njia ya kuiadhibu Uganda kwa kuiunga mkono serikali ya mpito ya Somalia.