Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu ya kuzuka tena mashambulizi ya kibaguzi yazuka Afrika Kusini:IOM

Hofu ya kuzuka tena mashambulizi ya kibaguzi yazuka Afrika Kusini:IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM hivi sasa linashirikiana na serikali ya Afrika ya Kusini, mashirika ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali nchini humo kujiandaa kuwaondoa wahamiaji wa Zimbabwe endapo kutazuka mashambulizi ya kibaguzi yaani xenophobia.

Hatua hiyo ni kutokana na hofu iliyotanda baada ya mashindano ya kombe la dunia ya kukazuka tena machafuko ya kibaguzi yanayolenga raia wa kigeni nchini Afrika Kusini. Kituo cha IOM kilichopo mpakani mwa Zimbabwe na Afrika Kusini mjini Beitbrige kimearifu kuwa idadi kubwa ya Wazimbabwe wameamua kurejea nyumbani kwa muda wakihofia machafuko.

Idadi kubwa ya raia wa kigeni wamearifiwa kukimbia nyumba zao katika wilaya za Nyanga, Philippi East na Khayelitsha na kuomba hifadhi kwenye kituo cha polisi kutokana na vitisho vya mashambulizi.