Skip to main content

Watu 64 wameuawa kwenye milipuko ya mabomu mjini Kampala Uganda

Watu 64 wameuawa kwenye milipuko ya mabomu mjini Kampala Uganda

Milipuko miwili ya mabomu imetokea mjini Kampaka Uganda jana usiku na kukatili maisha ya zaidi ya watu 60.

Mashambulio hayo yaliyotokea kwa kufuatana yalikumba mamia ya watu waliokuwa wameketi katika maeneo ya wazi wakiangalia fainali ya kombe la dunua kupitia runinga. Kwa mujibu wa maafisa wa polisi nchini Uganda kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Al-Shababu kutoka nchi jirani ya Somalia wanashukiwa kuhusika na shambulio hilo.

Na kama ndivyo basi hilo litakuwa ni shambulio la kwanza la kundi la Al-Shabab kufanyika nje ya ardhi ya Somalia. Umoja wa Afrika umesema shambulio hilo ni kitendo cha kigaidi na lazima kilaaniwe vikali.