Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya idadi ya watu duniani 2010 inaadhimishwa Julai 11

Siku ya idadi ya watu duniani 2010 inaadhimishwa Julai 11

Tarehe 11 Julai kila mwaka huadhimishwa siku ya idadi ya watu dauniani na mwaka huu 2010 kauli mbiu ni sensa yaani uhesabuji wa watu.

Nchi 60 duniani zinahesabu watu mwaka huu kama sehemu ya kushiriki siku hiyo, na takwimu zitakazokusanywa hazitosaidia tuu kujua ongezeko la idadi ya watu bali pia kutoa taarifa muhimu kwa ajili ya maendeleo ya mwanadamu. Katika kwenda sambamba na siku hiyo Radio ya Umoja wa Mataifa inaanza mfululizo wa makala maalumu iitwayo sensa njia ya kuelekea maisha bora. Katika makala hizo utasikia historia ya sensa na jukumu la Umoja wa Mataifa katika kuzisaidia nchi kukusanya takwimu .

Leo hii sensa haitumiki tena kwa kukusanya kodi na kuajiri, bali serikali zinatumia takwimu za sensa kama njia ya kijamii na kiuchumi katika kupanga mipango na mahitaji ya baadaye ya taifa. Mkurugenzi wa kitengo cha takwimu cha Umoja wa Mataifa Paul Cheung anasema anaamini kwamba takwimu sahihi ni muhimu sana katika kuunda sera za maendeleo.