Idadi ya wanaohitaji msaada wa chakula Niger na Mali imeongezeka:ICRC

Idadi ya wanaohitaji msaada wa chakula Niger na Mali imeongezeka:ICRC

Upungufu mkubwa wa chakula Niger na Mali umesababisha haja ya kuongeza mara tatu idadi ya wanaopokea msaada wa chakula kaskazini mwa nchi hizo.

ICRC inasema wakulima na wafugaji kaskazini mwa Mali na Niger wanakabiliwa na mchanganyiko wa matatizo ya chakula na mapigano ya kijamii. ICRC inasema miezi miwili iliyopita kulikuwa na haja ya kufikia watu 100,000 kwenye jimbo la Sahel ambako kunaishi wakulima na wafugaji.

Na tathimini ya sasa ni kwamba idadi ya wanaohitaji msaada imefikia mara tatu. Kama anavyofafanua Marcal Izard wa ICRC.

(SAUTI YA IZARD)