Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM na serikali ya Haiti wajiandaa na msimu wa kimbunga nchini humo

IOM na serikali ya Haiti wajiandaa na msimu wa kimbunga nchini humo

Msimu wa kimbunga kwa mwaka huu wa 2010 umetabiriwa kuwa utakuwa mbaya kabisa kuwahi kutokea nchini Haiti.

Serikali ya Haiti na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na jumuiya ya kimataifa wanafanya kila liwezekanalo kujiandaa na kimbunga hicho nchini Haiti. Mji wa Gonaives ndio ulio katika hatari zaidi ya kukumbwa na kimbunga Haiti , na umekubwa na mafuriko makubwa mawili katika kipindi cha miaka mine, yaliyosababisha watu zaidi ya 5000 wamepoteza maisha yao.

Kwa kushirikiana na uongozi wa eneo hilo ,programu ya IOM ijulikanayo kama PREPEP imekamilisha malazi ambayo yanahilimi kimbunga yaliyojengwa nje kidogo ya mji wa Gonaives yakiwa na uwezo wa kuhifadhi watu 500.