Skip to main content

Afrika itumie msukosuko wa uchumi kuingia kwenye uzalishaji:UNCTAD

Afrika itumie msukosuko wa uchumi kuingia kwenye uzalishaji:UNCTAD

Nchi za Afrika zimetakiwa kuchukua hatua kubalidi uchumi wake wakati zikichipuka tena kutoka kwenye mdororo wa uchumi, ili uweze kukuwa na kuwa imara katika siku za usoni kutkapozuka matatizo tena.

Hayo yamesemwa leo na wataalamu wanaohudhuria mkutano wa 50 wa bodi ya biashara na maendeleo TDB. Katibu mkuu wa UNCTAD na maafisa watatu wa uchumi wa Afrika wamesema mshituko wa masuala ya fedha ulioikumba dunia unalipa bara la Afrika sababu muhimu ya kubadili uchumi wake na kuhamia kwenye uwezo wa kiviwanda, kuimarisha miundombinu, kuimarisha uhusiano wa kikanda na kuboresha ushirikiano na nchi zilizoendelea.

Wataalamu hao wameongeza kuwa kufikia hatua hiyo kunahitaji kuimarisha hatua za serikali , kufufua masoko ya ndani na kushiriki katika biashara ya kimataifa. Wamesema hayo pamoja na msaada wa kimataifa na mchango mwingine wa kimataifa utalisaidia bara la Afrika kufikia malengo.