Fedha za dharura zinahitajika kuinusuru Afrika Magharibi:OCHA

Fedha za dharura zinahitajika kuinusuru Afrika Magharibi:OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesema mvua kubwa zilizonyesha mwezi wa Juni zimesababisha mafuriko na kupoteza maisha ya watu na mali zao Afrika ya Magharibi.

Msimu wa masika ulianza tangu mwezi Mai kwa baadhi ya nchi za Afrika ya Magharibi zikiwemo Benin, Ivory Coast, Ghana, Liberia, Niger na Togo.

Na mwezi mzima wa Juni OCHA inasema hakukuwa na fedha zozote zilizotolewa kusaidia watu walioathirika katika nchi hizo. Nchini Niger pekee watu milioni 7.1 na ukosefu wa chakula. Elizabeth Byrs ni msemaji wa OCHA

(SAUTI YA E BYRS))