Edward Norton ameteuliwa kuwa balozi mwema wa bayoanuai:UM

Edward Norton ameteuliwa kuwa balozi mwema wa bayoanuai:UM

Mwigizaji na mtengenezaji filamu maarufu ambaye aliwahi kushinda tuzo Edward Norton ameteuliwa kuwa balozi mwema wa bayoanuai.

Uteuzi huo ni ishara ya kuadhimisha mwaka huu wa 2010 kuwa ni mwaka wa kimataifa wa bayoanui. Bwana Norton ameiambia radio ya Umoja wa Mataifa kwamba mambo ambayo mabalozi wema wanaweza kufanya ni kutangaza shughuli ambazo zinaungwa mkono na Umoja wa mataifa na kutangaza mafanikio ili watu watambue jinsi binadamu walivyo na mchngo katika programu za mashirika ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI EDWARD NORTON)

Bwana Norton ana historia ndefu ya kusaidia masuala ya kulinda mazingira na viumbe na pia ni mjumbe wa bodi na muhamasishaji wa mfuko wa Wamasai wa kulinda maliasili ambao ni Wilderness Conservation Trust.