Kutofanyika mabadiliko kutakwamisha mambo muhimu Guinea-Bissau:Ban
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ripoti yake mpya amesema hatua zilizopigwa na Guinea-Bissau kufuatia mgogoro wa kisiasa wa mwaka jana ziko hatarini kama serikali haitofanyia mabadiliko masuala ya ulinzi na usalama.
Katika miezi ya karibuni nchi hiyo imeshuhudia ongezeko la mvutano wa kisiasa ambapo matukio mengi ya mauaji ya kisiasa yamefanyika mwaka jana na kutishia usalama na utulivu ambao ulipatikana baada ya uchaguzi wa Rais wa mwezi Juni mwaka 2009. Hata hivyo Ban amegusia katika ripoti yake maendeleo ya nchi hiyo na shughuli za ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kujenga amani UNIOGBIS.
Lakini amesema kuwekwa rumande kwa muda waziri mkuu wan chi hiyo , mkuu wa majeshi na maafisa wengine wa jeshi April mosi mwaka huu imekuwa ni pigo kubwa katika mchakato wa kurejesha hali ya amani na utulivu na utekelezaji wa mabadiliko muhimu.