Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wauzbek na Wakyrgy wakutana msikitini ili kusukuhisha tofauti zao

Wauzbek na Wakyrgy wakutana msikitini ili kusukuhisha tofauti zao

Watu zaidi ya miasita wamekutana msikitini karibu na mji wa Jalalabad Kusini mwa Kyrgystan katika juhudi za kupata maridhiano baiana ya jamii za Wauzbek na Wakyrgy.

Hatua hii imekuja baada ya kuzuka machafuko mwezi uliopita kwenye eneo la Kusini mwa Kyrgystan. Wazee wa Kyrgystan waliketi pamoja na jirani zao wa Uzbek wakinywa chai na kula matikiti maji huku wakijadili pamoja matumaini yao ya maisha bora ya siku za usoni. Viongozi hao wa jamii wametoa wito wa msamaha na kuahidi kuwafikisha kwenye mkono wa sheria waanzilishi wa ghasia zilizokatili maisha ya watu wengi na kuwaacha mamilioni kuwa wakimbizi.

Katika jamii ya Suzak nyumba nne tuu zilichomwa moto na kuathirika kidogo na machafuko, na jamii hiyo imetoa msaada kwa maelfu ya wakimbizi wa Jalalabad waliopita hapo kuelekea Uzbekistan. Wazee hao wanatumai kwamba mkutano wao utakuwa chanzo cha juhudi kubwa za kuchagiza amani nchini Kyrgystan. Akihutubia mkutano huo gavana wa Jalalabad Bektur Asanov amezihakikishia jamii zote kwamba serikali inafanya kila liwezekanalo kuwakamata na kuwachukulia hatua waliofanya machafuko.