Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haiti yaimarisha usalama wa chakula kutokana na msaada wa WFP

Haiti yaimarisha usalama wa chakula kutokana na msaada wa WFP

Miezi sita baada ya tetemeko baya zidi la ardhi Haiti iko njiani kujiimarisha katika usalama wa chakula kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP.

Inachofanya hivi sasa ni kujenga msingi imara wa lishe kwa watu wote walio na matatizo ya chakula katika nchi hiyo ya Carebean. Mkurugenzi mkuu wa WFP Josette Sheeran amesema saa chache baada ya tetemeko WFP ilikimbiza msaada wa dharura wa chakula uliosaidia nchi hiyo iliyosambaratishwa na tetemeko kutoingia katika tatizo lingine la njaa.

Lakini amesema kwa sasa wanashirikiana na serikali ya Haiti na wadau wengine katika programu ambayo ni ya mchanganyoiko wa chakula na fedha kwa kazi, chakula mashuleni na mradi wa lishe ili kujenga mfumo wa usalama wa chakula nchini Haiti.