Skip to main content

Uwajibikaji ndio nguzo katika kuwalinda raia kwenye migogoro:Ban

Uwajibikaji ndio nguzo katika kuwalinda raia kwenye migogoro:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kimoon aleliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa ubajibikaji ndio kitovu cha kuwalinda raia kwenye migogoro.

Amesema matukio yanayoendelea na hali ya hivi karibuni kama Kyrgystan, Gaza, Sudan, Sri Lanka, Somalia , Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kwengineko ,inatukumbusha kwamba kuwalinda raia kunasalia kuwa ni changamoto kubwa. Ban ameyasema hayo mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa mjadala kuhusu kuwalinda raia kwenye migogoro ya kutumia silaha.

Katibu Mkuu alijikita zaidi kwenye masuala ambayo ndio chanzo cha changamoto za kuwaweka raia msitari wa mbele katika ulinzi. Amesema kwanza ni kutumia ipasavyo vikosi vya kulinda amani, pili ni kushirikisha makundi yenye silaha katika ulinzi wa raia na tatu uwajibikaji ndio nguzo.