Maandamano yasababisha kufungwa ofisi ya UM nchini Sri Lanka

Maandamano yasababisha kufungwa ofisi ya UM nchini Sri Lanka

Ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Colombo nchini Sri Lanka zimefungwa baada ya maandamano. Ofisi hizo zimefungwa leo baada ya kiongozi mwenye msimamo mkali mshirika wa Rais wa Sri Lanka kuongoza maandamano makubwa nje ya ofisi hizo kwa siku ya pili akidai watakaa hapo hadi Katibu Mkuu Ban Ki-moon atakapolivunja jopo la uchunguzi wa uhalifu wa vita nchini humo.

Jana posili walilazimika kukabiliana na waandamanaji walioongozwa na waziri wa ujenzi na uhandisi Wimal Weerawansa, baada ya kuwazuia maafisa wa polisi kuwasindikiza nje ya jingo wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliokuwa wamekwama mjini Colombo.

Weerawansa ameahidi kwamba wafuasi wake wataingia kwenye mgomo wa kula kama Umoja wa Mataifa hautolivunja jopo hilo la uchunguzi. Mratibu wa Umoja w Mataifa nchini humo amesema leo hawakufanya kazi lakini anatumai kesho wataweza kuendelea na shughuli zao.