Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado kuna safari ndefu ili kila mtu aweze kupata huduma ya afya:Obaid

Bado kuna safari ndefu ili kila mtu aweze kupata huduma ya afya:Obaid

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA amesema bado kuna safari ndefu kuweza kufikia malengi ya kuwa na huduma ya afya kwa kila mtu.

Thoraya Obaid ameyasema hayo kwenye mkutano wa baraza la uchumi na jamii ECOSOC ambao umejadili mpango wa afya ujulikanao kama health 4+1. Mpango huo umekuwa ukishughulikiwa na UNFPA ikishirikiana na UNICEF, shirika la afya duniani WHO, Bank ya dunia na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na Ukimwi UNAIDS.

Nia ya mpango huo ni kuharakisha mchakato kwa ajili ya afya ya mama, watoto wachanga na watoto katika nchi 25 zinazopewa kipaumbele. Thoraya amesema kazi bado ipo kujitahidi kufikia malengo ya afya haswa afya ya uzazi. Ameongeza kuwa suala la afya ya watoto wachanga inatawala kwenye ajenda za kimataifa lakini msaada wa fedha zaidi unahitajika.