Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Malkia Elizabeth II amesisitiza amani na umoja alipohutubia UM leo

Malkia Elizabeth II amesisitiza amani na umoja alipohutubia UM leo

Malikia Elizabeth wa II wa Uingereza leo amehutubia Umoja wa Matifa ikiwa ni miaka 53 tangu aliposimama kwa mara ya kwanza mbele ya hadhira ya wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 1957.

Malikia Elizabeth mwenye umri wa miaka 84 hivi sasa, alikuwa na umri wa miaka 31 tuu alipohutubia UM, na ilikuwa ni miaka mine tuu tangu alipotawazwa na kuvishwa taji la kuwa malkia.

Malkia Elizabeth ambaye ameambatana na mumewe Prince Philip safari hii katika hotuba yake kwenye Umoja wa Mataifa ameupongeza Umoja wa Mataifa kwa juhudi kubwa unazofanya kwenye masuala mbalimbali na hasa amani, lakini akasisitiza ili kweli Umoja huo uwe Umoja wa Mataifa basi mshikamano ni muhimu sana.(SAUTI YA QUEEN ELIZABETH II)