Skip to main content

Pamoja na ulinzi UNAMID inawasaidia raia wa Darfur kupata maji safi

Pamoja na ulinzi UNAMID inawasaidia raia wa Darfur kupata maji safi

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID kwenye jimbo la Darfur ukiacha suala la ulinzi uko msitari wa mbele kuhakikisha watu wanapata maji safi.

UNAMID ina kitengo maalumu ndani ya mpango wake ambacho kinashughulika na suala la kuhakikisha wana nchi wa Darfur wanaosumbuliwa na adha nyingi wanapata maji safi ya kunywa na pia wanalinda mazingira.

Mkuu wa UNAMID wa masuala ya maji na ulinzi wa mazingira ni Emmanuel Molel amezungumza na mkuu wa Idhaa hii Flora Nducha na kumfafanulia kuhusu shughuli hiyo ya kuwapa maji raia wa Darfur Sudan.