Skip to main content

Ofisi ya Umoja wa Colombo Sri Lanka yazingirwa na waandamanaji

Ofisi ya Umoja wa Colombo Sri Lanka yazingirwa na waandamanaji

Waandamanaji wakiongozwa na waziri katika baraza la mawaziri la Sri Lanka wameizingira ofisi ya Umoja wa Mataifa hii leo.

Waandamanaji hao wanapinga jopo lililoundwa na Umoja wa Mataifa kuchunguza madai ya uhalifu wa vita nchini humo. Wimal Weerawansa ambaye ni waziri wa nyumba wa sri Lanka, alikuwa akipaza sauti na kutamka kauli za kupinga Umoja wa Mataifa wakati umati ulipovuka vizuizi vya polisi na kuandamana kwenye lango kuu la ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Colombo.

Waandamanaji hao waliokuwa wakidhibitiwa na polisi wa kutuliza ghasia walichoma picha ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.