Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM inahofia haki za wafungwa Cuba

Ofisi ya haki za binadamu ya UM inahofia haki za wafungwa Cuba

Ofisi ya kamishna mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa inasema imewasiliana na serikali ya Cuba kuhusu hali ya wafungwa nchini humo.

Barua kutoka kwa kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay ilitumwa Cuba mwezi April mwaka huu. Na Bi Pillay katika barua hiyo amesema anatiwa hofu na hali ya afya ya mfungwa Guillermo Farinas ambaye amekuwa katika mgomo wa kula.

Ameongeza kuwa masuala yaliyolalamikiwa na wafungwa nchini humo ikiwemo kunyimwa uhuru wa kushirikiana na uhuru wa kutembea ni mambo ambyo yanamtia hofu kubwa.