Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni muhimu kuwawezesha wanawake ili kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia: UM

Ni muhimu kuwawezesha wanawake ili kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia: UM

Hivi karibuni kitengo cha Umoja wa Mataifa la Jamii na Uchumi ECOSOC lilihitimisha majadiliano yake ya siku mbili na kutoa wito wa kuharakishwa kwa malengo ya maendeleo ifikapo mwaka 2015.

Katika mkutano huu, masuala ya akina mama yalipewa kipau mbele.

Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya UM alimhoji Hawa Ghasia, waziri wa nchi ya ofisi ya raisi, menegementi ya utumishi wa umma nchini Tanzania alipotembelea makau makuu ya UM kujadili suala hili.