Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vyama vya ushirika vitawasaidia akina mama

Vyama vya ushirika vitawasaidia akina mama

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kuwa akina mama katika mataifa mengi wanawezeshwa kuwa na fedha ya binafsi kupitia kwa vyama vya ushirika na hivyo kuwasaidia kupambana na dhana kuwa wanawake hawawezi kujisimamia.

Katika hotuba yake ya kusherehekea siku ya vyama vya ushirika duniani Ban ametaja usawa, kushirikishwa kwa wote katika hatua ya uamuzi, umiliki wa pamoja na kuwa na lengo lisilokuwa la kutengeneza faida kama baadhi ya manufaa ya kuwepo na vyama vya ushirika kwa akina mama duniani.

Katibu Mkuu amesema vyama vya ushirika ni muhimu sana hususan wakati huu wa hali ngumu ya kiuchumi duniani wa kupeana msaada kwa watu wasiojiweza katika jamii.