UNHCR kuomba mataifa zaidi kuanzisha mipango ya kuwapokea wakimbizi
Lengo la kuwahamisha wakimbizi katika mataifa mengine na idadi ya wakimbizi ambao mataifa wanakubali kuchukua itakuwa ajenda kuu katika mkutano wa pande tatu, serikali, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na Shirika la Umoja wa Mataifa ya kuwahudumia wakimbizi UNHCR, ambao utafanyika tarehe 6 hadi tarehe 8 mwezi huu.
Kwa wakimbizi wengi kuhamishwa hadi mataifa mengine itakuwa ndio njia ya pekee ya wao kuwa na suluhisho la kudumu kwa usalama wao sawa na kuwa na mahala pa kuishi milele.
Licha ya kurudi nyumbani kuwa njia inayopendekezwa kwa wengi wa wakimbizi duniani, mapigano ya mara kwa mara na hofu ya ukosefu wa uslama wao umewazuia wengi wao kukata tamaa ya kurudi mataifa walikotoka.
Zaidi ya elfu themanini ya wakimbizi wanaishi katika mataifa yanayoendelea ambapo wengo wao hawatasalia kwa amani.