Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima wanawake wawezeshwe ili kufikia malengo ya milenia:UM

Lazima wanawake wawezeshwe ili kufikia malengo ya milenia:UM

Umoja wa Mataifa na nchi wanachama wako katika mkakati kuhakikisha wanawake wanawezeshwa na kupata usawa wa kijinsia.

Kwa juma zima kumekuwa na mikutano mbalimbali kwenye makao makuu ya UM hapa New York ikijadili masuala ya kumuwezesha mwanamke na usawa wa kijinsia, pia ushirikishwaji wao katika utumishi wa umma katika harakati za kutaka kufikia malengo ya maendeleo ya milenia hapo 2015.

Wawakilishi kutoka nchi 50 wamehudhuria vikao hivyo mbalimbali na Tanzania ilikuwa miongoni mwao, na aliyeiwakilisha ni mbunge na waziri wan chi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma Hawa Ghasia. amezungumza na Flora Nducha kuhusu mkutano huo