Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ziara ya KM Ban Ki-moon nchini Gabon

Ziara ya KM Ban Ki-moon nchini Gabon

Masuala ya rushwa na uhifadhi wa mazingira yameongoza maongezi baina ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban-Ki-Moon na Rais wa Gabon Ali Bongo.

Katika mazungumzo yao Ban na Bongo vilevile walijadili hali ya mambo yalivyo kwa sasa katika nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati, mgogoro katika mpaka wa Gabon na nchi ya Equatorial Guinea na mchango wa Umoja wa Mataifa katika kulinda amani.

Aidha Ban amesifu jitihada za uongozi mzuri wa Gabon katika kufikia lengo la nane la maendeleo ya Milenia la kupingana na umasikini. Katika ziara hiyo kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa pia alihutubia Bunge la nchi hiyo na kusema Gabon ipo sambamba na Malengo ya Maendeleo ya Milenia, kwa kupunguza vifo vya watoto vinavyotokana na uzazi na uboreshwaji wa afya ya uzazi nchini humo.