Juhudi za kuunda serikali Nepal zinatakiwa zifanywe kwa haraka:KM

Juhudi za kuunda serikali Nepal zinatakiwa zifanywe kwa haraka:KM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Taifa Ban-Ki-Moon, amezitaka pande zote nchini Nepal kukubaliana kuunda Serikali kufuatia Kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Madhav Kumar Nepal.

Bunge la mpito liliundwa mwaka 2008, miaka miwili baada ya Serikali na kikundi kikubwa cha upinzani kukubaliana makubaliano ya amani, ili kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya muda mrefu, vilivyo gharimu maisha ya watu wapatao 13,000 nchini humo.