Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa ITU asisitiza umuhimu wa kurudisha haraka miundombinu ya mawasiliano Haiti

Mkuu wa ITU asisitiza umuhimu wa kurudisha haraka miundombinu ya mawasiliano Haiti

Harakati za kimataifa zinatarajia kuanza nchini Haiti, kuharakisha kuijenga upya miundombinu ya mawasiliano iliyoharibika kutokana na tetemeko la ardhi Januari 12, mwaka huu.

Mkutano uliojadili suala hilo mjini Barbados, ulihitimishwa kwa wajumbe kuweka nia thabiti kuhakikisha mawasiliano yanarudi nchini humo kwa kufanya kazi na Umoja wa Kimataifa wa Mawasiliano (ITU). Pamoja na misaada ya kibinadamu, wajumbe hao wameahidi msaada wa fedha kwenye Mfuko wa Haiti utakao anzishwa ndani ya ITU.

Katibu Mkuu wa (ITU), Hamadoun Tour'e, akizungumzia kuungana na juhudi za kimataifa kurudisha miundombinu ya mawasiliano iliyoharibiwa nchini Haiti, amesema suala hilo ni la haraka.