Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhamishaji waathirika wa tetemeko Haiti wakumbwa na tafrani

Uhamishaji waathirika wa tetemeko Haiti wakumbwa na tafrani

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema shughuli ya kuzihamisha familia zisizo na makazi nchini Haiti inatishiwa kukumbwa na ghasia kutokana na makundi ya wahalifu.

Kwa mujibu wa IOM shughuli ya kuzihamisha familia 263 mjini Port au Prince walioachwa bila makazi na tetemeko la ardhi la Januri mwaka huu imebidi ihairishwe na wafanyakazi wa IOM walitishiwa na makundi ya waliolipwa na wamiliki wa ardhi .

Familia hizo hivi sasa zinaishi katika hali mbaya. Kiwanja kikubwa cha mpira ambacho kinahifadhi watu wengi kimefurika maji machafu yaliyochanganyika na kinyesi na hivyo kutishia usalama na afya za wakimbizi hao wa ndani. Inakadiriwa kuwa watu milioni 1.5 bado hawana makazi miezi sita baada ya tetemeko la januari 12.