Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhumia Wakimbizi la UNHCR limepanda zaidi ya miti milioni 19 katika mpango maalum wa upandaji miti Kaskazini Mashariki wa Khartoum nchini Sudan.
Shughuli hiyo ilianza miaka 25 iliyopita. Shirika hilo limekuwa likijihusisha na mpango wa kulinda mazingira kwa nia ya kuwalinda na kuwasaidia wakimbizi wa Mashariki mwa Sudan, wakiwemo walioishi eneo hilo kwa zaidi ya Miaka 40. Maeneo ya mpakani mwa Sudan na Eritrie yanavutia kutoka na kuwepo miti iliyopandwa na UNHCR.
Toka miaka ya themanini, zaidi ya wakimbizi milioni moja toka Ethiopia na Eritrea wameishi katika zaidi ya kambi 12. Kutokana na watu wengi kuishi katika eneo hilo, kumesababisha uharibifu wa mazingira kwa watu hao kukata miti kwa ajili ya kuni. Mpango huo wa UNHCR ulishirikisha mashirika ya serikali na yasiyo yakiselikali nchini Sudan.