Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais Pierre Nkurunziza kuiongoza tena Burundi kwa muhula wa pili

Rais Pierre Nkurunziza kuiongoza tena Burundi kwa muhula wa pili

Nchini Burundi , Rais Pierre Nkurunziza pasina mshangao wowote , ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais iliofanyika siku ya jumatatu wiki hii.

Tume huru ya Uchaguzi imesema mtetezi huyo pekee katika uchaguzi kutoka chama tawala cha CNDD/FDD amejipatia ushindi wa kishindo wa asilimia 91 ya kura zote zilizopigwa.

Vyama vya upinzani vilivyojiondoa katika kinyang'anyiro hicho kwa madai kwamba uchaguzi wa awali wa madiwani ulighubikwa na wizi, vimesema havitoutambua utawala wa rais Nkurunziza . Kutoka Bujumbura, muandishi wetu Ramadhani KIBUGA anaarifu zaidi.