Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leo ni miaka 35 ya mkataba wa biashara ya viumbe vinavyotoweka

Leo ni miaka 35 ya mkataba wa biashara ya viumbe vinavyotoweka

Leo ni miaka 35 tangu kuridhiwa kwa mkataba kuhusu biashara ya kimataifa ya viumbe vilivyo katika hatari ya kutoweka yaani Flora na Fauna.

Katika ujumbe maalumu wa kuadhimisha siku hii CITES inasema kuanzia dawa hadi vifaa vya muziki na kuanzia fasheni na vipodozi, vyakula, na vifaa viingine vya vitukonavyo na wanyama na mimea, katika biashara lazima ifuatiliwe vyema kuhakikisha kuendelea kuishi kwa wanyama na mimea ya porini.

Katibu Mkuu wa CITES John Scanlon amesema wakati hakuna hata kiumbe kimoja kati ya 34,000 vilivyoorodheshwa na CITES kama viko hatarini kilichotoweka kutokana na mkataba wa biashara wa kimataifa hadi sasa, ongezeko la shinikizo malighafi za baolijia linafanya haja ya kufuatilia biashara ya kimataifa ya viumbe vya porrini kuwa muhimu sana wakati huu kuliko hata mwaka 1975 ambapo nchi ziliridia na kuanza kutekeleza mkataba huo wa kimataifa.