Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa chakula wa WFP sasa umevuka mpaka na kuingia Kyrgystan

Msaada wa chakula wa WFP sasa umevuka mpaka na kuingia Kyrgystan

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP linaendelea kugawa msaada kila siku kusini mwa Kyrgystan.

Juhudi zao zimeongezwa nguvu na kuwasili kwa malori kutoka nchi jirani ya Uzbekistan yakiwa yameshehemi misaada kwa ajili ya waathirika wa machafuko ya mwezi jana. Leo WFP imegawa msaada wa chakula kwa wtu 6300 katika soko kuu kwenye mji wa Osh kama sehemu ya mpango wake wa kugawa mlo kwa kila siku.

Kwa mujibu wa wafanyakazi wa WFP wakati wakifanya zoezi hilo soko lilikuwa wazi na kufurika watu, ikiwa ni ishara kwamba maisha yanaanza kurejea katika hali ya kawaida mjini humo.