ECOSOC yamaliza mkutano kwa wito wa kufikia malengo ya milenia

1 Julai 2010

Baraza la jamii na uchumi ECOSOC limehitimisha majadiliano yake ya siku mbili ya ushirikiano wa maendeleo kwa wito wa haja ya haraka ya kuwa na mipango ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia hapo 2015.

Pia imetaka kuwa na uelewa wa maeneo ambayo kufikia malengo kutakuwa na athari iwe ni kwa kuwekeza kwa wanawake na wasichana au kusaidia uwezo wa kugawanya rasilimali za jamii. Rais wa baraza hilo Hamidon Ali wa kutoka Malaysia amesisitiza haja ya uwiano baina ya ushirikiano wa maendeleo na mambo ambayo ni zaidi ya msaada , sera za biashara, uwekezaji na teknolojia utashi wa kisiasa wa wahisani.

Amesema wahisani lazima waweke malengo kwa mwaka 2011 hadi 2015 wakati wa mkutano wa mwezi Septemba utakaotathmini hatua zilizopigwa kufikia malengo ya milenia.

(SAUTI YA HAMIDON)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter