Mwigizaji maarufu azungumzia umuhimu wa mwanamke katika jamii

30 Juni 2010

Mwigizaji mashuhuri ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Academy ya nchini Marekani, Geena Davis amevitaka vyombo vya habari kuonesha umuhimu wa mwanamke katika jamii ili kufikia lengo la nane la maendeleo ya milenia, ifikapo mwaka 2015.

Davis amesisitiza shauri hilo wakati akihutubia moja ya mikutano ya mwaka ya baraza la uchumi na jamii la Umoja wa Mataifa, huku akionyesha kuridhishwa na juhudi za Umoja wa Mataifa katika kukuza maendeleo ya kiuchumi na kupambana na unyanyasaji dhidi ya wanawake duniani.

Bi Davis amesema kwa kipindi kirefu vyombo vya habari vimetoa picha mbaya kwa mwanamke, jambo ambalo linaathiri vizazi vijavyo kuamini mwanamke anastahili nafasi za chini katika jamii. Davis amesisitiza kuwa kama hakutakuwa na jitihada za makusudi, hali hii itarudisha nyuma juhudi zinazo fanywa kumkomboa mwanamke.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter