Afisa wa UM amekaribisha kuteuliwa kwa bodi huru nchini Sudan

30 Juni 2010

Kiongozi wa tume maalum ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan, ameikaribisha bodi huru iliyoteuliwa kusimamia maandalizi ya kura ya maani ambayo itashuhudia kujitenga ama la, kwa Sudan Kusini.

Haile Menkerios ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ameipongeza Kamati hiyo ambayo imepitishwa na bunge la Sudan kusimamia mchakato wa kura ya maoni Sudan ya Kusini. Kura ya maoni ya kujitenga ama la kwa Sudan ya Kusini imepangwa kufanyika Januari mwakani ambapo itakuwa mwisho wa mpango wa makubaliano ya amani (CPA) ya mwaka 2005.

Katika taarifa yake, Menkerios amezitaka pande zote kufanikisha madhumuni ya kuleta amani nchini Sudan. Tume hiyo huru inawajibika kutoa msaada wa kiufundi na kitaalamu kwa pande zote zinazoshiriki mpango huo wa kura ya maoni.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter