Baraza la usalama limeongeza muda wa kikosi chake nchini Ivory Coast

30 Juni 2010

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limeongeza muda wa mpango wa shughuli zake nchini Ivory Coast.

Mpango huo UNOCI unaungwa mkono na majeshi ya Ufaransa katika juhudi za la umoja wa Mataifa kurejesha utulivu na amani katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi. Operesheni za UNOCI sasa zitaendelea hadi mwishoni mwa mwaka huu. Baraza hilo kwa pamoja lilipitisha azimio bila kupingwa na kuipa UNOCI na vikosi vya Ufaransa jukumu la kufuatilia makundi yenye silaha Ivory Coast, kulinda raia, kulinda haki za binadamu hususani za watoto na wanawake, kutoa msaada wa kibinadamu na kutafuatilia vikwazo vya silaha nchini humo , utachagiza pia mchakato wa masuala ya amani.

UNOCI pia imepewa jukumu la kusaidia katika maandalizi ya kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki, uchaguzi ambao umekuwa ukiahirishwa mara kadhaa na kuchangia katika shughuli ya kuwapa vitambulisho raia. Mbali ya hayo UNOCI ina wajibu wa kuendelea kuchangia katika utekelezaji wa mchakato wa amani kwa kunga mkono upokonyaji silaha, kuwaingiza kwenye jeshi la serikali wapiganaji waasi, kuhifadhi silaha zinazorejeshwa na pia kusaidia kituo maalumu cha kuwasaidia waasi wa zamani.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter