Shambulio la kombora hospitali Moghadishu lauwa mgonjwa na kujeruhi

30 Juni 2010

Hospitali ya Keysaney kaskazini mwa Moghadishu nchini Somalia, jana ilishambuliwa kwa kombora ambayo yaliua mgonjwa mmoja na kumjeruhi mwingine.

Kombora hilo lilitua kwenye moja ya jengo ya hospitali hiyo linalotoa huduma ya dharura kwa majeruhi wa vita. Mbali ya kuua mgonjwa paa ya jengo hilo iliharibiwa vibaya na kuweka nyufa kubwa kwenye kuta na kuiacha hospitali katika hali mbaya zaidi.

Kombora hilo lilivurumishwa licha ya hospitali hiyo kuwekwa nembo kubwa ya msalaba mwekundu. Rais wa jumuiya ya msalaba mwekundu nchini Somalia Dr Ahmed Mohamed Hassan amesema tuna wasiwasi mkubwa kuhusu wagonjwa na wafanyakazi katika hospitali ya Keysaney, hali inakuwa mbaya zaidi wakati ambapo watu wanaona hawawezi kupata hata usalama hospitali.

Ameongeza kuwa huduma inyotolewa na hospitali ya Keysaney ni muhimu sana na ICRC imezitaka pande zote husika katika mapigano kuzingatia wajibu wao wa kutowashambulia wahudumu wa afya, hospitali, zahanati na majengo mengine kama hayo.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter