Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya mambo nchini Kyrygystan bado haitabiriki inasema UNICEF

Hali ya mambo nchini Kyrygystan bado haitabiriki inasema UNICEF

Mwakilishi maalumu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF nchini Kyrgystan anasema hali ya mambo bado ni tete.

Mwakilishi huyo Jonathan Veitch anasema hali haitabiriki na bado kuna hofu kubwa ingawa watu wengi waliokimbilia nchi jirani ya Uzbekistan wamerejea nyumbani . UNICEF na mashirika mengine wametumia rasilimali zao kutoa msaada kwa maelfu ya waathirika wa machafuko na sasa yanategemea jumuiya ya kimataifa kutoa msaada.

Amesema watu kati ya 300,000 na 400,000 waliokimbia wamerejea Kyrgystan. Ameongeza kuwa hofu sasa ni kulindwa kwa watu hao na hasa watoto.

(SAUTI YA JONATHAN VEITCH)